Siasa za Msitu wa Mau zaleta Tumbo joto, Uko familia zaidi ya 60 zikiofia kufurushwa

0
279

Huku serikali ikijiandaa kutekeleza awamu ya pili ya kuwaondoa watu ambao wangali kwenye msitu wa Masai Mau kinyume cha sheria, familia zaidi ya 60 kutoka jamii ya wamaasai ambazo zimekuwa zikiishi sehemu ya msitu huo zimesalimu amri na kujiondoa kabla ya serikali kuanza kuwaondoa.

Familia hizo zimekuwa zikiishi katika mashamba yaliyoko Enkaroni Group Ranch katika msitu huo wa Masai Mau.Zikiongozwa na mzee Moses Ole Kiok ambaye amekuwa akimiliki ekari 80 katika sehemu ya msitu huo anasema wameamua kutii amri ya serikali ya kuwataka wao waondoke katika msitu kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

READ MORE :  Stay Away! Police Warn As Gvn Sonko set to be arraigned in court

Aidha, wameweza kuondoka pamoja na mifugo wao na hapo akawataka watu ambao wangali kwenye msitu huo kutii amri hiyo ya serikali na pia kuondoka kwa minajili ya kuhifadhi msitu huo ambao wanasema sio muhimu tu kwa taifa la Kenya bali ukanda wote wa afrika mashariki.

Kadhalika, wametaka pia wanasiasa kukoma kuingiza siasa swala la msitu wa Masai Mau huku wakisisitiza kwamba japo wengine wao hawana mashamba kwingine wameamua kutoka ndani ya msitu na kutafuta makao kwa majirani sawa na kwa jamaa zao kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.

Comments