MWANAUME AJITIA KITANZI KITENGELA, UKO UCHUNGUZI UKIANZISHWA

0
179

Wenyeji wa mtaa cha’ngombe katika mji wa Kitengela kaunti ya Kajiado wameamkia taarifa za taanzia baada ya mwanaume mmoja kupatikana amejitia kitanzi asubuhi ya leo nyumbani kwake.

Kulinga na majirani walioshuudia tukio hilo wanasema mke wa mwenda zake ndiye alikuwa wa kwanza kubaini kutopotea kwa mumewe nyumbani, jambo ambalo si la kawaida na alipowaarifu majirani wakaanza kumtafuta , na muda mfupi baade akapatikana amejinyonga Juu ya nyumba yao, kwenye orofa ya kwanza.

READ MORE :  Kitui former Senator vengeance book to be launched Amid calls to stop it

Majirana hao ambao wamewachwa vinywa wazi baada ya kitendo hicho wanasema tukio hilo limewapata kwa mshtuko mkubwa kwani mwanaume huyo hakuwa na ugomvi na mtu yeyote na uhenda alijitia kitanzi kutokana na msongo wa mawazo.

Kadhaliki wamesisitiza haja ye yeyote kuweka wazi kile kinacho msumbua badala ya kuchukua hatua ya kujitoa uhai, Tayari polisi wameondoa mwili wa mwenda zake na kupeleka katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya shalom huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Comments