Hali ya wasi wasi yakumba kijiji cha Matungu, Bugoma

0
87

SHARE WITH US


Hali ya wasiwasi na huzuni imeghubika kijiji cha Nanyeni eneo bunge la Matungu kufuatia kisa ambapo mwanafunzi wa darasa la saba anakisiwa kunajisiwa na kuuawa kabla ya washukiwa kuteketeza nyumba alimokuwa amelala usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na wazazi wake mwendazake mwenye umri wa miaka 15, marehemu hulala jikoni na walighutushwa na moshi pamoja na mwanga mkali wa moto na kutoka nje ndipo walipata jiko hilo linateketea.

Wanadai waliingia na kujaribu kumuokoa mwana wao wakidhani alikuwa amezirai kwa sababu ya moshi huo ila walibaini alikuwa amenyongwa kutumia nguo.

Aidha, Hadija chibayi mamake marehemu anadai mwana wao alinajisiwa kwani nguo zake za ndani zilizokuwa kando na mwili wake zilikuwa zimejaa damu.

Andrew werimo ni mwalimu mkuu wa smule ya msingi ya nanyeni alikokuwa akisoma

mwalimu mkuu akizungumza nasi kwa njia ya simu OCPD rabai matsili amedhibitisha kisa hicho akidai walimpata akitokwa damu kwa masikio, mdomo na hakukuwa na majeraha yeyote mwilini na kuwa wanasubiri ripoti ya upasuaji

Mwili umepelekwa katika hospitali kuu ya bungoma ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

SHARE WITH US