ABIRIWA WAKWAMA UKU USAFIRI UKITATISWA ENEO LA KAJIADO

0
52

Abiria wanaosafiri kuelekea Tanzania wamelazimikia kusitisha safari yao na kukimbilia Usalam wao katika kituo cha polisi cha bissili baada ya wenyeji wa wa eneo hilo kufunga barabara wakilalamikia ajali ya jana usiku ambapo basi la kampuni ya Dar Lux liligongana na gari la probox na kuwaua watu waili papo hapo.

Abiria hao ambao walikuwa wakisafiri kutoka hapa Jinini Nairobi kuelekea nchini Tanzania walijipata kwenye kizasaa hicho kwanza saa 12 asubhui baada ya wenyeji waliokuwa na ghadhubu ambao wanalalamikia misururu ya ajali ambayo yamekuwa yakisababishwa na mabasi hayo kufunga barabara na kusababisha mabasi hayo kutafuta usalama kwa polisi wakisubiri barabara ifunguliwe.

Wakaazia wa Ngatataeka ambao wamefunga barabara wanadai licha ya madereva husika kuzingati sheria za trafiki wakiwa nchini Tanzania, wanapoingia kwenye barabara za humu nchini utepetvu unasheheni kwa upande wao.

Kamanda wa polisi katika eneo la Kajaido ya kati Isa Muhamud anasema tayari Polisi wamefika katika eneo hilo kutuliza hali, huku shuguli zikitarajiwa kurejelewa wakati wowote kwanzia sasa.

Hata hivyo abiria waliokuwa kwenye basi lillohusika kwenye ajali ya usiku wa kuamkia leo walilazimka kukesha kwenye kijibaridi, kwani hadi sasa basi hilo halijaondolewa barabarani wala abiri hao kutafutia mbinu mbadala ya usafiri.

Comments
Previous articleEx lover Kills Woman, Attempts to Take Own Life in Kitui
Next articlePolice in Emali disperse irate Boda Boda demonstrators
For Any breaking news, Exposee's, Gossips, Human Interest articles or interesting videos, share with us, Videos and pictures can be sent to +254727132802 on WhatsApp, and Telegram. Email us: bonyoana@gamail.com